Bila shaka unakumbuka enzi zileee. Unamtokea mrembo, kwa uchumba au urafiki tu wa kawaida wa mapenzi(hauruhusiwi kabisa enzi hizo lakini weeh..nani awe wa kwanza kumpiga mwenzie jiwe!). Anakuja kwenye miadi. Anang’ata kucha, anarembua, mguu unachezeshwa weee mpaka kinatokea kishimo. Maua yanachumwa mpaka lile la mwisho kabisa. Unaimba ngonjera zako na mashairi yako yote. Mwisho anakupa jibu; ngoja nikafikirie.Damn! Safari bado ni ndefu kumbe. Unaanza mwendo wa barua,mwendo wa zawadi za peremende nk.Bado tu!
Mara enzi zikaanza kubadilika. Ikawa badala ya miaka miwili ikawa ni mwaka mmoja. Kisha ikawa miezi sita, mwezi mmoja na sasa….hapo weka jibu lako mwenyewe. Heka heka za siku hizi wenyewe wanakwambia usipime. Sio wanaume wala wanawake. Ili mradi tu ni fujo tupu.
Sasa Fid Q akimshirikisha Matonya wanakuja na “shule,onyo,ombi”.Hata sijui niiteje. Wimbo unaitwa Usinikubali Haraka. Hivi kwani kunani jamani kama mwenyewe ndio keshakamatwa na ile inayoitwa “Love at First Sight”? Sikiliza wimbo huu halafu sema usikike. Heko kwa Fid Q na Matonya kwa wimbo huu kwani ni wazi kuna ujumbe na mjadala ndani yake.Wimbo umepikwa pale MJ Records au maarufu kama kwa Master J.
1 comment:
Acha kukopi materials za wenzako wewe na usiseme umetoa wapi.Hii umeiba BC.Na nitamwambia mwenyewe...shenzi wee
Post a Comment