Mwimbaji nyota wa muziki wa kizazi kipya,Joseph Haule maarufu kama Professor Jay,anajiandaa kutengeneza video ya track zake za Nang'atuka na Sauti ya Gheto zilizopo kwenye albam yake ya Aluta Kontinua.Kwa mujibu wa Jay,kazi hiyo itakamilika baada ya muda sio mrefu ujao na itafanywa na kampuni maarufu ya Visual Lab...."Nipo katika matayarisho ya mwisho nianze shooting...mategemeo yangu kwamba itakuwa project nzuri itayowavutia mashabiki kama inavyotokea kila mara ninapofanya kazi na Visual Lab" alisema.Albam ya Aluta Kontinua ambayo ilizinduliwa kwa kishindo miezi michache bado inaendelea kutambulishwa kwa mashabiki wake wa mikoa mbalimbali kazi ambayo hata hivyo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment