Sunday, June 14, 2009

DJ CHOKA HAJAGOMBANA NA PROF.JAY.

Ni mengi wiki iliyopita yalitanda ndani ya vyombo vya habari kuwa Dj Choka ametafautiana na Prof.Jay,E! Xtra link ilipata kuzungumza na Dj Choka alisema "Hizo habari ni za kizushi kabisa na mimi sijagombana na Prof.Jay na kamwe sitofanaya hivyo,kwani Jeezy ni kaka yangu pia tumeanza kufanya kazi pamoja kwa kitambo.Hayo ni maneno ya kizushi tu.Nilichosema kuwa kwamba kama kuna msanii yoyote ambaye atataka nimpigie kwenye show yake ni fedha tu ndio inayozunguza.Mimi nipo na Prof.Jay kama uji na mgonjwa,Pia najua ni mengi yanazungumzwa na yanaendelea kuzungumzwa ila mashabiki wajue ukweli ndio huo sina tofauti na Prof.Jay".Kwa upande wa E! Link ilijaribu kumtafuta Prof.Jay alisema "Kusema ukweli ameshtushwa na huo uvumi ndio maana mpaka sasa hajuamua kuongea na vyombo vya habari,kifupi ni kwamba yeye na Dj.Choka wapo pamoja si kama vile waandishi wanavyofikiria kwani Choka ni mdogo wangu ambaye tumekuwa bega kwa bega kila siku".

HABARI NDIO HIYOOOOOOOO.............!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

No comments:


I made this widget at MyFlashFetish.com.