Mabeste & Pancho Latino (Mwenye headphone)
Jina la Pancho masikioni si geni sana,ni moja kati ya Producer ambao wafanya vizuri katika kupika beat zilizojaa ufundi wa hali ya juu.Pancho wameshatengeneza nyimbo kibao kama vile "Baby Candy","Watasimulia" za Prince Dully Sykes,"Ngoma itambae" ya Chid Benzino ambaye ni mwaka mwaka huu ilichukua Tuzo za Kilimanjaro Music Awards.Pancho alianza katika studio za Dhahabu Record akahamia Kiri Record na kwa sasa yupo ndani ya studio za B-Hitz Music Group akishirikiana na Hermy B ambaye mwaka huu amechukua Tuzo ya Producer bora.Pancho ni kijana mwenye umri mdogo anatengeneza beat ambazo zinamzidi umri,kijana kusema ukweli anatisha.Sasa ameshafanya na wasanii kama vile A.Y,Prof.Jay,Naakaya na wengine wengi ndani ya studio za B-Hitz.
WENGI MTAULIZA JINSI YA KUMPATA PANCHO NI VIPI?
Pancho anapatikana katika studio za;
B-HITZ MUSIC GROUP
KINONDONI-VIJANA MTAA WA HOME ALONE
NAMBA YA SIMU NI: +255 755 893232
KAMA WEWE NI MSANII NJOO UPATE KWA MUZIKI MZURI KWA BEI NZURI TU...!!
No comments:
Post a Comment