Wednesday, July 9, 2008

RAY C SASA YUPO KAMILI.


Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rehema Chalamila almaarufu kama Ray C, ameibuka na kusema sasa amerudi upya akiwa na kibao chake kisemacho ‘Nihurumie Wangu’ ambacho tayari kimeshaanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari wetu hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Ray C, alisema kwamba kimya chake cha muda mrefu hakikuwa kikimaanisha amekufa kimuziki kama baadhi ya mashabiki walivyoanza kudhania, bali alikuwa anasoma muziki na jinsi ya soko linavyokwenda kwa sasa, huku akitoa nafasi kwa chipukizi nao kuonesha vipaji vyao.“Sio siku zote upende kusikika wewe peke yako, ni vema kuwapisha na wengine ili kuweza kuonesha uwezo wao katika ‘gemu’, sasa nimekuja upya katika jumba la mapambano, hakuna kulala bali mambo yote ni mbele kwa mbele,” alisema Ray C.Aidha, mwanamuziki huyo ambaye pia ni maarufu kama ‘Sinyorita’ au ‘Kiuno bila Mfupa’ alisema kuwa ujio wake huo ni moja ya mikakati ya kuandaa albamu mpya ambayo alidai kuwa itasheheni nyimbo lukuki zilizo simama imara huku akiwashirikisha wasanii maarufu kibao wa ndani na nje ya nchi.Ray C alisema kwamba amejifunza mambo mengi katika muziki. Hiyo inatokana na kufanikiwa kufanya maonesho mbalimbali katika nchi za Sweden, Uingereza na Marekani na kusema ziara hizo zilimwezesha kupata mwangaza mkubwa katika sanaa ya muziki.

No comments:


I made this widget at MyFlashFetish.com.